Aliyekuwa Nahodha na Beki wa Timu ya Taifa ya England John Terry yuko mbioni kujiunga na Al-Shabab FC ya Saudi Arabia ili kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya ligi kuu nchini humo.

Gwiji huyo wa Chelsea amekuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Pro League na tayari mkataba wa kuwa kocha mpya klabuni hapo umekubaliwa kwa maneno.

Na ikiwa itafanikiwa, Terry atajiunga na orodha ya majina mengine makubwa kutoka Premier kuhamia katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Terry mwenye umri wa miaka 42 kwa sasa, alifuatwa na mabosi wa AI-Shabab karibu mwezi mmoja uliopita na amepewa kandarasi ya miaka miwili na hadi kufikia minne.

Kwa sasa anafanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mshauri katika kituo cha kukuza na kuendeleza vijana cha Klabu ya Chelsea.

Msimu uliopita Terry alifanya kazi chini ya kocha Dean Smith kwenye klabu ya Leicester City na Aston Villa lakini anatamani kuwa kocha mkuu kwa sasa.

Gamondi amuandaa Skudu kuivaa El Merrikh
Ongezeko la Talaka: Kamati zashauri elimu ya ndoa mapema