Mrembo Jokate Mwegelo amepata shavu la kuwa mtangazaji ‘Talk Show’ mpya itayorushwa kwenye channel za Star Times.

Jokate ambaye amefanya kazi za utangazaji na vituo vikubwa vya runinga Afrika, anatarajiwa kuwa nyota ya kuing’arisha ‘Talk Show’ hiyo iliyopewa jina la Mashariki Max itakayolenga katika kuonesha utamaduni wa maisha ya Afrika Mashariki.

“Nimekuwa nikihost shows nyingi, lakini naamini Mashariki Max itanipa uzoefu zaidi na itanisaidia katika career yangu kwa sababu watu wengi wataniona kwa sababu show itarushwa na Star Times kupitia ST Swahili Channel,” Jokate aliwaambia waandishi wa habari.

Kipindi hicho kitakachotumia lugha ya Kiswahili, kitaanza kurushwa hivi karibuni kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu.

Jokate ni mtangazaji wa vipindi vya runinga mwenye vipaji vingi ikiwa ni pamoja na uigizaji, uimbaji na urimbwende.

Audio: Nuru The Light Arejea Na Wimbo Mpya Wenye Herufi Moja ‘L’
De Bruyne Ampeleka Draxler VfL Wolfsburg