Kiungo wa kimataifa wa England, Jordan Henderson amekiri pesa ndio ilikuwa sababu mojawapo ya kujiunga na Al- Ettifaq kutoka Saudi Arabia.
Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool, 32, anasema aliumia alipozomewa na mashabiki wa Uingereza ambao hawakufurahishwa na hatua yake ya kuhamia Saudi Arabia.
Lakini anadai kumekuwa na mkanganyiko kuhusu nia ya uhamisho wake wa Pauni 700,000 kwa wiki baada ya kuonekana kwamba alikwenda Saudia kwa ajili ya pesa tu.
Kiungo huyo alikiambia Kituo cha Televisheni cha Channel 4 amedumu kabla ya England ya kushinda 3-1 dhidi Italia Jumanne usiku: “Nilifanya mahojiano miezi michache iliyopita na labda baadhi ya mambo niliyosema yalichukuliwa vibaya.
Mfano ningesema nimekwenda Saudia sio kwa sababu ya pesa. Nadhani itakuwa tofauti kubwa sana. Sio jambo la kushangaza kwa sababu nimekwenda kwa ajili ya pesa.” alisema Henderson.
Mwezi uliopita kiungo huo aliwaomba radhi mashabiki kwa sababu anaamini amesababisha taharuki alipohamia Saudia katika dirisha la usajili la kiangazi.
Baada ya kuichezea England mechi 80 katika historia yake ya soka alisema: “Nadhani kuwa na mchezaji kama mimi kutokana na thamani yangu itakuwa jambo zuri sana kwa Saudi Arabia.
Kabla sijaenda Saudia thamani yangu haijabadilika, sasa wananifikiria vibaya eti kwa sababu nimekwenda nchi nyingine.”