Nahodha na Kiungo wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Jordan Henderson anaamini klabu hiyo inapaswa kuwatumia wafungaji mabao wote waliopo kwa manufaa yao msimu ujao 2023/24.

Kurejea katika utimamu wa Luis Diaz katika wiki za hivi karibuni kunamaanisha Meneja Jurgen Klopp sasa anaweza kuchagua kati ya washambuliaji watano kati ya sita ambao ni chaguo la kwanza (Roberto Firmino anayeondoka ni majeruhi).

Hilo limechangia kuimarika kwa kiwango ambacho kimeleta ushindi mara sita mfululizo na kuwafanya waingie katika kuwania nne bora, wakiwa pointi moja nyuma ya Manchester United ambao wamecheza mechi moja zaidi.

Ikiwa wachezaji hao Mohamed Salah, Darwin Nunez, Diogo Jota, Cody Gakpo na Diaz wanaweza kubaki fiti, Henderson anatarajia Liverpool kuimarika kwa kiwango kikubwa msimu ujao.

“Mambo yanabadilika kila wakati na tumekuwa na wachezaji wapya wanaokuja kwenye safu hiyo ya mbele na ni wachezaji wa kufurahisha sana,” amesema akiambia Sky Sports.

“Kuna vitu vingi tofauti tunaweza kutumia na wachezaji tofauti ambao wanaweza kufanya mambo to tauti kweli.

“Tuna wachezaji wengi wenye ubora ambao wanaweza kwenda mbele na wote wanaweza kufunga mabao, hivyo tunahitaji kuwatumia kwa manufaa msimu ujao.

“Limekuwa jambo la kusisimua kwetu msimu huu kuwa waaminifu labda tumejitahidi kupata uthabit kwa walio wengi.

“Jambo zuri ni kwamba tunafa nana zaidi na sisi na nadhani bado kuna safari ndefu ya kuboresha kwetu lakini dalili ni nzuri.

“Natumaini tunaweza kumaliz mechi hizi tatu kwa nguvu zaidi.”

Maridhiano na Serikali: CHADEMA, Lissu watofautiana
Madai ya Membe kwa Msigwa yapo palepale - Wakili