Beki wa kulia wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Jordi Alba ana matumaini ya kumuona kiungo mshambuliaji wa Chelsea Pedro Rodriguez anarejea katika klabu hiyo.

Beki huyo aliyasema hayo jijini Paris nchini Ufaransa alipokuwa Akizungumzia mchezo wao wa pili dhidi ya Uturuki utakaopigwa kesho katika muendelezo wa michuano ya Euro inayofanyika nchini Ufaransa.

Kiungo huyo wa Chelsea aliondoka Nou Camp mwaka jana lakini ameongea na Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bertomeu kuhusu uwezekano wa kurejea kwa miamba hiyo ya Catalunya.

“Ni rafiki mzuri, ametengeneza historia akiwa na Barcelona natamani kumuona akirudi hapa.

“Tunashirikiana mambo mengi, alichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Barcelona ya sasa, ni matumaini yangu atarejea tena”.

” Alituacha mwaka uliopita lakini ni vyema akarejea tena, ni thamani kubwa kwa timu kuwa na mchezaji kama Pedro” alimalizia Alba.

Wote Alba na Pedro walikuwepo katika kikosi cha Hispania kilichoshinda mchezo wa kwanza wa michuano ya Euro katika kundi D dhidi ya Jamhuri ya Czech siku ya Jumatatu kwa goli 1-0.

Simba SC Kumuajiri Kocha Aliyetwaa Kombe La Dunia
Video: Gwajima awindwa. Majanga matano uzimaji wa simu feki. Mkapa jipu kuu - Magazeti leo