Mwimbaji wa ‘No Air’, Jordin Spark ameingia kwenye mgogoro na Billboard baada ya kuandika kichwa cha habari kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake wa zamani, Jason Derulo huku ikiacha lengo kuu ambalo ni kutangaza ujio wake mpya.

Habari iliyowekwa kwenye mtandao wa Billboard ilikuwa na kichwa cha habari ‘rdin Sparks on the ‘Pain and Confusion’ From Her Breakup With Jason Derulo.”

Baada ya kuchukizwa na kichwa hicho cha habari, mwimbaji huyo aliamua kuwaelekeza jinsi walivyopaswa kuandika kichwa cha habari ambacho kingetoa habari chanya kwa muziki wa Jordin Spark.

“I made a better headline 4 you! MT @Billboard: Jordin Sparks on her biggest comeback fear ‘the landscape has changed,’ Jordin alitweet.

Jordin Spark ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na rapa Sage the Gemini, amerudi tena kwenye muziki ambapo Agosti 21 aliachia albam yake mpya ya ‘Right Here Right Now’.

Album hiyo inaifuatia album ya ‘Battlefied’ iliyotoka mwaka 2007 na kufanya vizuri.

Serena Williams Kumaliza 2015 Akiwa Kileleni?
Baada Ya Benzema, Sasa Ni Cavani