Mshambuliaji machachari wa FC Barcelona Lionel Messi yupo tayari kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Baba wa mshambuliaji huyo, amewathibitishia mashabiki wa mwanae, kufuatia hofu iliyotanda baada ya soka la nchini China kuibuka kwa kasi na kuwateka baadhi ya wachezaji mashuhuri duniani.
Jorge Messi, baba wa Lionel Messi, amesema hana wasiwasi kuhusu suala la mtoto wake kusaini mkataba mpya, zaidi ya kusubiri muda utakapowadia.
Amesema kwa sasa shughuli za kukamilisha masuala ya mkataba huo bado yanaendelea, kwa pande mbili kujadiliana na imefikia mahala pazuri.
Uongozi wa FC Barcelona juzi ulionyesha kuhofia zogo la usajili la klabu za nchini China, na kutangaza kusitisha mpango wa kuweka baadhi ya mambo hadharani.
Messi ameitumikia FC Barcelona kwa zaidi ya miaka kumi, baada ya kupandishwa katika kikosi cha kwanza mwaka 2004.
Kati ya 2003–2004 Messi alikuwa mchezaji wa kikosi cha Barcelona C na B.
Mpaka sasa ameshaitumikia FC Barcelona katika michezo 363 na amefunga mabao 326.