Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) wameripotiwa kumpigia hesabu beki wa kati wa Atletico Madrid, Jose Gimenez ili iweze kutatua tatizo lake katika safu ya ulinzi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, tayari makachero wa klabu hiyo ya The Gunners wapo kwenye mazungumzo na nyota huyo kuona kama wataweza kumpata kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Jose Gimenez ni sehemu tu ya mawindo ya Arsenal ambayo pia inamwania beki wa Valencia Shkodran Mustafi na beki wa zamani wa Manchester United Jonny Evans.

Arsenal inataka kunasa mmoja kati ya mabeki hao watatu lakini hadi sasa juhudi zao zinakwamishwa na bei mbaya za nyota hao.

Valencia imesema Mustafi hataondoka bila pauni milioni 42 huku bei ya Evans ikitajwa kufikia pauni milioni 25.

Claudio Ranieri Apandwa Jeuri, Ni Baada Ya Kuyabakisha Majembe Yake
Mamadou Sakho Arejea Mazoezini Liverpool