Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amethibitisha kwa vitendo kutokua na mapenzi na klabu ya Chelsea ambayo aliitumikia kwa vipindi viwili tofauti.

Mourinho alionyesha hali hiyo kwa kukataa kusaini jezi ya klabu ya Chelsea mara baada ya kuwasili nchini China, ambapo kikosi cha mashetani wekundu kimekwenda kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya nchini England.

Meneja huyo kutomka nchini Ureno, alipokelewa kwa shangwe na mashabiki waliojitokeza kuwalaki Man Utd wapowasili nchini China lakini miongoni mwao walikuwepo mashabiki wa Chelsea.

Kama ilivyo kawaida kila shabiki alitaka kubaki na kumbu kumbu ya saini ya meneja huyo pamoja na za wachezaji wengine wa Man Utd, lakini cha kushangaza Mourinho alionekana kusaini jezi za Man Utd na kuziacha zile za Chelsea jambo ambalo lilizua gumzo.

Hata hivyo Mourinho hakusema jambo lolote kuhusu kitendo hicho na badala yake alijikita kuzungumzia mchezo wao wa kirafiki ambao watapambana na Borussia Dortmund hii leo na kisha Manchester City siku ya jumapili.

Jose Mourinho alilazimika kuondoka Chelsea mwishoni mwa mwaka 2015, baada ya kutakiwa na uongozi wa klabu hiyo kufanya hivyo, kutokana na matokeo mabaya yaliyomuandama katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini England msimu wa 2015/16.

Luis Enrique: Ni Wakati Sahihi Kwa Messi Kustaafu
Alipwa kubikiri wasichana, wazazi wamkabidhi watoto wao na kufanya sherehe