Leo kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kwaajili ya kuanza majukumu yake kunako klabu hiyo.
Katika mkutano huo, Mourinho ametumia dakika zote tano kurusha vijembe kwa hasimu wake mkuu Arsene Wenger.
Mourinho amekuwa na mahusiano mabaya na Arsene Wenger kwa miaka mingi na hata kufika wakati kumpachika jina la ‘mtaalam wa kufeli’ kutokana na kushindwa kuchukua taji la EPL tangu mwaka 2004.
Kijembe hicho alikirusha baada ya kuulizwa ana kipi cha kuuthibitishia ulimwengu ubora wake kwa mara nyingine kufuatia kufukuzwa na Chelsea December mwaka jana.
Mourinho akajibu: “Kuna baadhi ya mameneja, imepita miaka kumi wakiwa na timu zao bila kuchukua taji la lgi, ni mwaka mmoja tu umepita tangu mimi kuchukua taji hili,”amesema.
“Nahisi natakiwa kuthibitisha hili, sio kwa watu wengi bali kwangu mimi mwenyewe. Kamwe sitaweza kufanya kazi isiyo na mafanikio. Hiyo ndiyo asili yangu.
“Kama nina lolote la kuthibitisha, hebu fikiria kwa wengine, kwangu mimi kumaliza nafasi ya nne sio lengo.”
Mourinho amekeiri kwamba amejisikia faraja kubwa kuwa kocha wa klabu kubwa kama United.
“Kati ya awamu zote nilirudi hapa. Hii ina utofauti. Nilifukuzwa na Chelsea na nikabaki hapa hapa na kuwa naonana na sura zile zile kila siku,” amesema.
“Ni vigumu sana kuelezea. Napata wakati mgumu sana kutafuta maneno sahihi ya kuielezea klabu hii.
“Hii ndoto kubwa niliyokuwa nikiota kla siku, na hatimaye imekamilika. Nimekuwa rasmi meneja wa Manchester United. Hii ni fursa ambayo kila mtu angependa kuipata.”
Vile vile Mourinho amesema anatambua fika kwamba nini hasa mashabiki wa timu hiyo wanataka.
“Nafahamu wajibu wangu, nafahamu matarajio ya wengi, na nafahamu pia historia na ya timu hii,”ameongeza. “Najua nini kinanikabili, na najua nini hasa mashabiki wanachotarajia kutoka kwangu.
“Changamoto hii hainifanyi niwe na hofu yoyote kwasababu historia yangu kwa zaidi ya miaka kumi inajieleza.
“Hii ni nafasi ambayo imekuja kwa wakati muafaka katika maisha yangu ya kufundisha soka. Najisikia niko imara na mwenye hamasa kubwa. Nipo sehemu ambayo nilihitaji kuwepo kwa sasa.”

 

Video: Kamanda Sirro ampongeza Mwanamke shujaa, Ulinzi wakutosha Eid el Fitr
Polisi Kuwasaka Boda Boda Wasiovaa Kofia Ngumu