Rais wa FC Barcelona, Josep Maria Bartomeu amekanusha hatua ya kuwasilishwa kwa ofa inayomlenga mshambuliaji wa klabu hiyo, Pedro Eliezer Rodríguez Ledesma ambaye anahusishwa na taarifa za kuwindwa na Man Utd.

Bartomeu ambaye alichaguliwa kuendelea kuiongoza FC Barcelona mwishoni mwa juma lililopita baada ya kukaimu kiti cha urais kufuatia kujiuzulu kwa Sandro Rosel, amesema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiudanganya umma kwa kuripoti kuwa wamepokea ofa ya paund milioni 22 kutoka Old Trafford.

Amesema taarifa hizo hazina ukweli kwani mpaka sasa hakuna yoyote ambaye ameshasikia wala kuona ofa inayomuhusu mshambuliaji huyo ambaye anashinikiza kuondoka kutokana na changamoto zinazomkabili katika kikosi cha kwanza.

Pedro amekuwa na wakati mgumu wa kuwania nafasi ya kucheza kila juma kutokana na uwepo wa washambuliaji nguli kama Lionel Messi, Neymar pamoja na Luis Suarez, hatua ambayo ilipelekea kucheza michezo 15 tu, msimu uliopita.

Van Persie Aikabidhi Familia Yake Fenerbahce
Nyota Ya Uingereza Yamuwakia Abou Diaby Wa Arsenal