Beki wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Croatia, Josko Gvardiol, yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la kujiunga na Manchester City kwa ada ya uhamisho ya Pauni 86 milioni ambayo itamfanya kuwa beki ghali zaidi duniani.

Kwa sasa beki ghali duniani anabaki kuwa Harry Maguire wa Manchester United aliyetua katika timu hiyo akitokea Leicester City miaka minne iliyopita kwa dau la Pauni 80 milioni.

Dili Joskoi mwenye umri wa miaka 21, linatarajiwa kukamilika juma hili kwani makubaliano yote yameshafanyika huku ikiwa inasubiriwa ruhusa ya staa huyu kusafiri hadi England kwa ajili ya fanyiwa vipimo vya afya.

Josko ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027, msimu uliopita alicheza mechi 41 za michuano yote.

Nyota huyo ambaye mara kadhaa amehitajika Chelsea kuziba pengo la Kalidou Koulibaly, ameonekana kuvutiwa zaidi na ofa ya Man City kwa sababu anaamini ataenda kushinda mataji.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola katika ripoti yake ya usajili kwa msimu ujao alijumuisha jina la staa huyu kwani anaamini eneo la ulinzi linahitaji ‘mtu’.

Melis Medo aagiza usajili wa Majimengi
Usajili Azam FC wamshutua Feisal Salum