Mabingwa wa kuchekesha, Ze Comedy wanaoishikilia rekodi ya wachekeshaji waliotazamwa sana kwenye TV nchini Tanzania kupitia kipindi chao pendwa cha Ze Comedy mpaka Orijino Komedi, wapo mbioni mwaka huu kurudi kazini.
Ni muda mrefu sasa, Orijino Komedi haijarushwa kwenye runinga, kitu ambacho kimepelekea mashabiki wengi wa kipindi hiko kuhoji maswali mengi yasiyo na majibu. Vyombo vya habari vliichukua jitihada za kumsaka mmoja wa wachekeshaji hao, baada ya kumpata Joti ambaye alieleza kinagaubaga sababu za wao kutokuwa kazini.
‘Kama kundi tuna taratibu zetu na ndio maana tumejaribu kutumia muda wa mwaka mmoja kupumzika maana toka tuanze kufanya kazi hatujawahi kupumzika, tulivyopumzika pia sio kukaa kimya tukaangalia project za kila mtu binafsi na ndio maana unaona kila mtu na shughuli zake‘ – Joti
‘Ukimfatilia Mpoki kuna shughuli zake anafanya na inajulikana, Masanja pia vivyo hivyo… na mimi nimefungua Youtube channel yangu ya Joti TV, nafikiri mwaka huu tunaweza kurudi kazini pia amesema Joti.
Wachekeshaji hawa ni kati ya watu ambao sanaa yao imewatambulisha vizuri sokoni, hata katika kila shughulli wanazojihusisha mbali na uchekeshaji jamii hupokea vyema na kukiamini, ni wasanii wachache sana Tanzania ambao wameza kuhimili katika sanaa ya uchekesahji na ikawatoa kiuchumi.
Japo wengi wanajaribu lakini sio kwa kiwango ambacho kundi la Ze Comedy wamekifanya, hivyo wapenzi watazamaji wa wachekeshaji hawa wakae tayari mwaka huu Ze Comedy kuingia mzigoni, hivyo wajiandae kuvunja mbavu kwa mambo mazuri watakayokuja nayo.