Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeeleza kuongezeka kwa joto juu ya wastani kufikia nyuzi joto 34 na litadumu mpaka Januari mwakani kutokana na kuwapo kwa jua la utosi na mvua hafifu za vuli.
Meneja wa kituo kikuu cha Utabili, Samweli Mbuya ameeleza sababu ya kuongezeka kwa joto ni mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa kusini mwa mstari wa Ikweta na kusababisha jua la utosi katika mwezi Novemba, Desemba, na Januari.
Sababu nyingine ni mtawanyiko wa mvua za vuli hafifu, hivyo kusababisha jua la utosi ambalo ni kawaida kwa nyakati hizi ,na kusababisha ongezeko la joto katika maeneo mbalimbali hususani kanda ya pwani.
Mbuya ameeongeza kuwa baadhi ya maeneo ya nchi mvua zimenyesha za wastani lakini sehemu nyingi ni chini ya wastani na kwa muda ulio salia hakutarajiwi kiwango cha mvua kuongezeka bali, zitanyesha za wastani na chini ya wastani.
Aidha amewataka wannchi kufuatilia taarifa za mwenendo wa joto zinazoendeleakutolewa katuka utabiri wa kilasiku na TMA na kuchukua hatua stahiki kila inapobidi.