Pambano wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting ambalo litachezwa hii leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, limeonyesha kuwa na hisia za ushindani kufuatia tambo zinazoendelea kutolewa katika mitandao ya kijamii.

Mapema hii leo, afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire aliandika ujumbe ambao unadhihirisha joto la mpambano huo kuendelea kupanda kwa kiasi kikubwa, kufuatia kuthibitisha kufika kwenye uwanja wa Uhuru mishale ya alfajiri.

WhatsApp Image 2016-09-07 at 08.09.49Masau Bwire akiwa uwanja wa Uhuru mapema hii leo.

Ujumbe ulioandikwa na Masau Bwire.

Habari za asubuhi wapendwa ndugu zangu wote humu ndani….

Mimi ni mzima, namshukuru kuniamsha salama siku hii ya leo yenye historia kubwa kwangu mimi, timu yangu ya Ruvu Shooting, Wadau, wapenzi na washabiki wa Soka.

Leo katika uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, Simba ya Dar es salaam inaumana na timu chachali Ruvu Shooting ya Pwani. Ni historia inaandikwa leo katika medani ya soka Tanzania pale dakika 90 za mchezo huo zitakapohitimishwa na mwamuzi bora Ngole Mwangole.

Tangu saa 11 alfajiri niko hapa Uwanja wa Uhuru, lakini wapo pia wa upande wa pili ambao wakati nafika nimewakuta! Wapo hapa Wazee wawili tunatazamana!

Tunafanya nini, hayakuhusu, tuachieni wenyewe!

Video: JPM afichua utapeli Magomeni Kota, Amshukuru mzee wa CUF
Nape ataka wasanii hawa watengwe