Beki wa zamani wa Manchester United Nemanja Vidic ameondoka Inter Milan na anafikiria kujiunga na ligi ya Marekani MLS (Daily Mail).

Manchester United sasa wanamfuatilia kiungo wa Valencia Andre Gomes baada ya meneja wa Atletico Madrid Diego Simione kukataa kumuuza Saul Niguez (Daily Star).

Bournemouth wanamtaka winga wa QPR Matt Phillips anayesakwa pia na West Brom (Sun).

Real Madrid na Barcelona wameungana na Manchester City kutaka kumsajili kiungo wa Schalke, Leroy Sane, 20, ambaye bei yake ni pauni milioni 40 (Daily Mirror).

Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini anasema hatotafuti beki wa kuziba pengo la Vincent Kompany, ingawa mchezaji huyo huenda asirejee hivi karibuni (Guardian).

Arsenal wanakaribia kuwasajili vijana wawili kutoka Nigeria, Kelechi Nwakali na Samuel Chukwueze waliowika kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya cini ya miaka 17 mwaka jana (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia anataka kumuongeza mkataba Joel Campbell (Daily Telegraph).

Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge, baada ya kuanza kunyatiwa na Inter Milan na Fiorentina (Sun).

Meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema kutokana na majeruhi katika ushambuliaji, huenda akataka kumsajili Saido Berahino kutoka West Brom (Daily Express), ikishindkana Hiddink pia anaweza kumsajili jamie Vardy au Emmanuel Adebayor (Times).

Sunderland wanafikiria kuongeza dau kutaka kumsajili beki kutoka Ivory Coast Lamine Kone anayeichezea Lorient (Chrinicle).

Leicester City wapo tayari kumpa mkataba mpya beki wa kushoto Ben Chilwell na kuongeza mshahara wake wa pauni 800 kwa wiki ili kuzuia asinyatiwe na Arsenal na Liverpool wanaomtaka (Daily Mail).

Meneja wa Stoke City Mark Hughes ametupilia mbali taarifa kuwa mshambuliaji wake Marko Arnautovic anataka mshahara wa pauni 100,000 kwa wili ili aaini mkataba mpya (Soke Sentinel).

Mshambuliaji wa West Ham Nikica Jelavic anatazamia kuondoka na kujiunga na Guangzhou Evergrande ya China (Evening Standard).

Mshambuliaji wa Watford Alessandro Diamante anajiandaa kujiunga na Atalanta ya Italia kwa mkopo (Watford Observer).

Azam FC Waingia Kambini
Louis Van Gaal Awalaumu Wachezaji Wa Man Utd