Aliyekuwa mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Prince Ali bin Al Hussein amempinga rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini kwa kusema hafai kusimama katika kinyang’anyiro cha kujaza nafasi ya Sepp Blatter kwenye uchaguzi wa mwezi februari mwakani.

Ali bin Al Hussein ambaye ni mtoto wa mfalme wa Jordan, ametoa angalizo hilo baada ya saa 24 kupita baada ya Platini kutangaza nia ya kuwania kiti cha uraisi wa FIFA akipata baraka kutoka kwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya UEFA mwishoni mwa juma lililopita.

Al Hussein amesema Platini hana sifa zilizo thabiti za kuiongoza FIFA ambayo kwa sasa imetapakaa uchafu wa rushwa, hivyo amewataka wadau wa soka duniani kutambua kwamba kuna ulazima kwa baadhi ya viongozi kujipima kabla ya kutangaza nia ya kuwania nafasi kubwa katika taasisi za kidunia.

Hata hivyo Al Hussein hakueleza kwa nini anadhani Platini hatoshi katika nafasi hiyo kwa vigezo vya kuzuia rushwa, zaidi ya kusisitiza kuwa kuna ulazima kwa baadhi ya watu kujichunguza kwanza kutokana na vitendo vinavyoendelea miongoni mwa watu wanaowazunguuka.

Katika hatua nyingine Al Hussein, bado hajatangaza kama atawania nafasi ya urais kwa mara nyingine tena ama la, hali ambayo inahisiwa huenda ikawa ni hofu kwake baada ya kuona Platini ametangaza nia ya kukitaka kiti cha urais wa FIFA.

Herve Renard Amvuta Tena Sunzu Ufaransa
Xavi Amuomba Jambo Muhimu Guardiola