Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania, (Tanrods) kuweka alama ya X katika jengo la Shirika la Umeme (Tanesco) na sehemu ya jengo la Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kupisha ujenzi wa daraja la juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange).

Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo hii leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili kutoka Chato Mkoani Geita alikokwenda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda.

Amewataka Tanrods kuwapa taarifa wahusika kuhusu kubomolewa kwa majengo yao ili wapate eneo lakutosha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo unaolenga kupunguza foleni katika jiji la Dar es salaam.

“Sasa mimi nataka ikiwezekana leo au kesho muweke alama ya X, jengo la Tanesco na sehemu ya mwanzo ya majengo ya Wizara ya Maji,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Aidha, amesema kuwa sheria ya hifadhi ya barabara ilianzishwa mwaka 1932 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1959, 1964, na 1967.

Hata hivyo, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Magufuli akiwa waziri wa Ujenzi aliagiza kubomolewa kwa jengo la Tanesco Ubungo, hata hivyo aliyekuwa Waziri Mkuu wa kipindi hicho, Mizengo Pinda alizuia kubomolewa kwa jengo hilo.

Donge nono la mil. 10 lamuibua kigogo Takukuru
Grace Mugabe atimkia Namibia