Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania pia mgombea urais kupitia chama cha Mapiduzi Dkt. John Magufuli amelitaka jeshi la Polisi mkoani Kagera kumuachia mkuu wa shule ya ya msingi Byamungu wakati jeshi hilo likiendelea kufanya Uchunguzi.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akiongea na wananchi wa mkoa wa Kagera katika kampeni ambapo amesema kuwa hata akiwa nje ya mahabusu ataendelea kushirikiana na jeshi la polisi wakati jeshi jilo likiendelea na uchunguzi.

‘’Mkuu wa mkoa ninaomba huyo baba nina uhakika mkuu wa shule hana moyo mmbaya hivyo wa kuchoma hao watoto,  alianzisha shule kwa ajili ya kusoma hawa watoto wetu, ningeomba awe nje ya lock up hizo za polisi kwa sababu tunamuongezea mateso mengine mbali ya mateso ya kupotelewa watoto hao kumi ambao aliwalea kama watoto wake,” amesema Magufuli.

Itakumbukwa Usiku wa kuamkia Septemba 14, 2020 shule hiyo ilipata ajali ya kuungua kwa jengo ambalo lilipelekea wanafunzi 10 kupoteza maisha  na wengine kujeruhiwa.

Biashara United Mara waijibu Simba SC
Biashara Utd kazi wanayo, Manara asema mazito

Comments

comments