Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino aliyoianzisha wakati wa ibada ya uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Emmaculata.

Harambee hiyo ameifanya kwa lengo la kuhakikisha Makao Makuu ya nchi yanakuwa ni sehemu ambayo imezungukwa na uwepo wa Mungu, ambapo ameeleza kuwa Msikiti wa Chamwino bado ni mdogo hivyo ipo haja ya kuchangia ili uweze kuwa mkubwa.

Mahali ambapo ni Makao Makuu ni lazima pazungu kwe na watu wanaomtukuza Mungu, Baba Askofu kama utaniruhusu na hili nakuomba sana, basi tutumie siku ya leo pia tuchange tuanze kujenga Msikiti wa ndugu zetu Waislamu ambao Msikiti wao ni mdogo na wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu na baadhi ya wasaidizi wangu ni Waislamu na yupo anaitwa Alhaji na ameshaenda kuhiji“,¬†amesema Rais Magufuli.

“Tutamuomba Baba Paroko angalau akaziwasilishwe kwa Sheikh kwenye Msikiti wetu na tutajipanga taratibu namna ya kuanza kuukarabati, tukimaliza tutaendelea tena kwenye Kanisa lingine”.

Katika harambee hiyo aliyoifanya Rais Magufuli, amekusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 48, ambapo pia imetolewa mifuko ya Saruji pamoja na michanga.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 24, 2020
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 23, 2020