Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameambatana na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kuhudhuria tukio la kuapishwa kwa Cyril Ramaphosa hapo kesho.
Katika safari hiyo, Rais Magufuli pia ameungana na makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM), Philipo Mangula na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.
Aidha, katika safari hiyo, Prof. Kabudi amesema kuwa baada ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa atafanya ziara maalumu nchini Namibia ambako atazindua mnara uliopewa jina la baba wa taifa Hayati, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua umuhimu wa mchango wake.