Leo tarehe 19 Januari 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watano ambao wataiwakilisha nchi katika balozi za nchi mbalimbali.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ameawataja mabalozi walioteuliwa na vituo vyao vya kazi, ni pamoja na Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ambaye ataiwakilisha Tanzania katika ubalozi wa Beijing China.
Vile vile amemteua George Kahema Madafa ataiwakilisha Tanzania Rome Italy, Balozi Emmanuel John Nchimbi ataiwakilishi nchi Brasil Brazil, Balozi Fatma M Rajab ambae ataiwakilisha nchi Doha Qatar.
Wengine ni Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ambaye ataiwakilisha Tanzania Ankara nchini Uturuki na Balozi Dkt. James Alex Msekela ambae ataiwakilisha nchi Geneva-Umoja wa Mataifa.
Aidha, Mabalozi hao wanatarajiwa kuapishwa kesho tarehe 20 Januari 2017 saa 10:30 jioni Ikulu Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, Rais Magufuli amemteua Muhidin Ally Mboweto kuwa balozi ambapo tarehe ya kuapishwa na sehemu ya kazi atapangiwa baadaye.