Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ameanza kunyoosha mfumo wa uongozi ndani ya chama hicho kwa kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Muhimu kwa lengo la kubana matumizi na kuongeza ufanisi.

Kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) kilichokaa jana chini ya uenyekiti wake, kimepunguza idadi ya wajumbe wa Halmashauri hiyo kutoka 388 hadi 158.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM anayemaliza muda wake, Nape Nnauye, Kikao hicho pia kiliridhia kupunguza idadi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kutoka 34 hadi 24 na kwamba kutakuwa na wajumbe watatu wa kuchaguli wa NEC kutoka Bara na Watatu kutoka Zanzibar, mbali na wajumbe wanaoingia kutokana na nyadhifa zao.

Aidha, kikao hicho kilipunguza idadi ya vikao vya kamati zote za chama hicho ili kupunguza mzigo wa gharama za uendeshaji wa vikao ndani ya chama hicho.

Kikao hicho pia kilipunguza wajumbe wa kamati ya siasa ngazi ya wilaya kwa kuwaondoa katibu wa uchumi wa fedha, katibu wa kamati ya madiwani na wajumbe wawili wa kuchaguliwa na halmashauri ambapo jumla yao watakuwa wanne tu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli amemteua Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey Polepole kuwa Katibu Itikadi na Uenezi akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Nape Nnauye.

Wastaafu 332 wasotea mafao yao muhimbili
Bosi mtandao wa jamii forums mbaroni