Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuachana na makampuni yaliyopeleka barua za maombi ya kununua zao la Korosho.
Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kuwaapisha Mwaziri na Manaibu Waziri, ambapo amesema kuwa Korosho zote zilizopo mikoa ya kusini itanunuliwa na serikali.
Amesema kuwa hakuna haja ya kuwauzia wafanyabiashara hao kwakua Korosho hiyo itanunuliwa kwa shilingi 3300 badala ya 3001.
“Hawa wanaokuja hawa watatuletea matatizo tu, huku wakulima wetu wakihangaika, korosho zote zitanunuliwa na serikali, na mpaka sasa wanajeshi wameshajiandaa, na wako tayari kwenye maghala wanalinda,”amesema JPM