Rais Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Kilimo ijitathmini kutokana na suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea pamoja na utendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania.
Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kumrudisha wizarani Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Prof. Wakuru Magigi baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.
Ametoa agizo hilo katika kikao chake na wakuu wa mikoa inayolima korosho kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
“Haturidhishwi na utendaji wa bodi ambao umekiuka maelekezo ya msingi ya Serikali katika kusimamia mfumo mzima wa zao la korosho uliopelekea kuvurugika kwa minada.”amesema Majaliwa
Aidha, kutokana na hali hiyo, Majaliwa amesema kuwa Serikali imesitisha minada yote ya korosho nchini kuanzia leo na kuwataka wakulima wawe watulivu wakati ikishughulikia suala hilo.
-
TPA yawataka Wahandisi kuchangamkia fursa
-
Makonda amvutia kasi Amber Rutty, amtaka ajisalimishe polisi
-
Serikali yamkaanga Wema Sepetu
Pia Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli anataarifa kwamba kuna baadhi ya watendaji Serikalini wanatumia vibaya jina lake kwamba lazima wahusika wote watachukuliwa hatua.
Hata hivyo, awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi walilalamikia kitendo cha Prof. Magigi kuvuruga mfumo wa uuzaji wa korosho.