Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo tarehe 19 Januari 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Martin Bille Herman Ikulu Jijini Dar es salaam.
Aidha, mazungumzo hayo yamehudhriwa na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard, na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Martin Bille amesema kuwa katika mazungumzo hayo wamejadiliana kuhusu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na kukubaliana kuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo na uchumi.
Vilevile, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amesema kuwa lengo la kukutana na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.