Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli, ametuma salamu za pole pamoja na rambirambi ya shilingi milioni tano kwa familia ya Mlelwa, kufuatia mauaji na kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa Emmanuel Mlelwa.

Akitoa salamu za pole katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wilayani Ludewa mkoani Njombe, Katibu wa NEC Uchumi na fedha wa Chama hicho ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Njombe, Dokta Frank Hawasi, amesema Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha kijana huyo kutokana na umuhimu wake kwa familia na taifa.

“Mwenyekiti wetu amepokea taarifa ya kifo cha kijana wetu Emmanuel Mlelwa kwa masikitiko makubwa sana, kwa sababu sio kifo cha kawaida, lakini pia umuhimu wa kijana mwenyewe kwa nchi kwa ujumla,” amesema Hawasi.

 “Mwenyekiti wa CCM Taifa analaani kitendo kilichofanyika kwa ndugu yetu Emmanuel Mlelwa kwa sababu hakionyeshi utu, hakionyeshi uzalendo na hakionyeshi utanzania wetu ”ameongeza Hawasi

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa kupitia kwa katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama hicho taifa Dkt. Frank Hawasi, ameagiza vyombo vya Dola mkoani Njombe kuwatafuta na kuwabaini waliohusika na mauaji ya Emmanuel Mlelwa.

Mwambusi: Ulikua mpango maalum kumuanzisha Carlinhos
Tshabalala ataja kilichoiokoa Gwambia FC