Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempandisha cheo Kaimu Meneja wa Kampuni ya huduma za Meli (MSCL), Erick Hamis kuwa Meneja mkuu kwa kile alichodai kuwa amependezwa na mikakati yake inayoonyesha dhahiri nia yake ya kulifufua shirika hilo na kumpa sharti la kutolewa sifa na kuliua tena shirika.

Amefika uamuzi huo wakati akihutubia wananchi na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Mwanza baada ya kushuhudia makubaliano rasmi ya mkataba wa ujenzi wa Meli mpya Chelezo, na ukarabati wa Meli za MV Victoria na MV Butiama katika ziwa Victoria na kampuni nne kutoka Korea Kusini, mkataba ambao una thamani ya Shilingi bilioni 152.

Aidha, amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikielekea mwisho na alikuwa mbioni kuifuta kama sio jitihada za kiongozi huyo kuonyesha nia katika kupambana na rushwa ambayo ndio kikwazo alichokitaja kuwa vyanzo vya mapato, hivyo kumuagiza meneja huyo kuhakikisha hakuna kitakachopotea kuanzia leo anapokabidhiwa majukumu rasmi.

“Enzi zile kulikuwa na wizi, wafanyakazi walikuwa wakiiba mafuta. Mapato yalipokuwa yakipatikana yalikuwa yakipelekwa Dar es Salaam na wafanyakazi wanafahamu”. Rais Dkt. Magufuli.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa meli hiyo mpya na ukarabati wa meli nyingine za MV Victoria na Mv Butiama na ujenzi wa Chelezo, Meneja huyo amesema ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 yenye tani 400 utatoa ajira 250

 

IGP Sirro afanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa
Ronaldo de Lima kuimiliki Real Valladolid