Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo, Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, leo, Septemba 12, 2019, Rais Magufuli amemuapisha mkuu huyo mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa na amemtaka kuchapa kazi na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Msuya amechukua nafasi ya Dkt. Modestus Kapilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Neema yaendelea kudhihiri TFF, yasaini mkataba ya mabilioni
Ilibaki kidogo Pogba aondoke Old Trafford