Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya(Drug Control and Enforcement Authority).
Uteuzi huo umefanyika leo Februari 10, 2017 na Kamishna huyo atasaidiwa Mihayo Msikile ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick Kibuta  ambaye anakuwa Kamishna wa Intelijensia.
Pia, Rais magufuli amemteua Dkt. Anna Peter Makalala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Taarifa hizo kutoka Ikulu zimeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Dkt. Anna Makalala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Aidha, taarifa hizo zimeeleza kuwa wateule wote wataapishwa Jumapili Februari 12, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam