Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA), Dkt. Irene Isaka.

Dkt. Isaka ameondolewa siku moja baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari kutetea kikokotoo kipya kinachompa mstaafu mkupuo wa 25% za mafao yake, tofauti na 50% za awali.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Dkt. Isaka atapangiwa kazi nyingine na kwamba uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa Mamlaka hiyo utafanyika baadaye.

Uamuzi wa Rais Magufuli umekuja saa chache baada ya kumaliza kikao alichofanya Ikulu na wawakilishi wa wafanyakazi; pamoja na viongozi wa Serikali ambao ni pamoja na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Joakim Mhagama, Dkt. Isaka aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kikao hicho, Rais Magufuli alielekeza kuwa kikokotoo kipya kilichopo kwenye kanuni mpya kinachotoa asilimia 25% kisitishwe na kwamba kikotoo cha zamani kiendelee kwa kipindi cha mpito cha hadi mwaka 2023.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 29, 2018
Viongozi 9 wa upinzani watiwa mbaroni Sudan

Comments

comments