Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema atafanya uteuzi wa Naibu Waziri mwingine wa Madini baada ya aliyemteua, Francis Kumba Ndulane, kushindwa kuapa leo Jumatano Desemba 9, 2020.

Rais Magufuli amesema hilo akizungumza mara baada ya zoezi la uapisho na Manaibu Waziri aliowateua hivi karibuni, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma. 

Kumba ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini alikuwa mmoja wa waliotakiwa kuapa lakini alikuwa akishindwa kutamka maneno na kutakiwa kukaa pembeni ili wenzake waendelee kuapa.

“Wote nimewaangalia na hata wewe uliyeshindwa kuapa tutateua mtu mwingine anayeweza kuapa vizuri, najua waziri Mkuu ananiangalia kwa sababu Lindi wametoka yeye na huyo aliyeshindwa kuapa, sasa tutamteua mwingine na huyu tutacheki Degree yake vizuri, ” amesema Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, Ndulane ana elimu ya shahada ya uzamili katika uhasibu na fedha ambayo ameisomea katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 na 2015. Pia, ana stashahada ya juu ya uhasibu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).

Ndulani alisoma shule ya msingi Uwanjani (mwaka 1980 – 1986), baadaye akaenda sekondari ya Tambaza (mwaka 1987 – 1990) na baada ya kuhitimu kidato cha nne, alikwenda sekondari ya Pugu (mwaka 1991 – 1993).

Magufuli amtaka Jafo kumtumbua Mkurugenzi Geita
JPM awaapisha Mawaziri wapya