Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia wizara ya Nishati, ametoa kiasi cha shilingi bilioni 210 kwaajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa Umeme unaojengwa mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani kwenye ziara yake ya siku tatu mkoani Ruvuma, ambapo amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa fedha hizo kwa kushirikiana na wahisani wengine.

“Mheshimiwa Rais ndio ametoa fedha hizi bilioni 210 kwa kushirikiana na wahisani ambapo bilioni 104 ni kwaajili ya kusambaza umeme katika wilaya zote za mikoa ya Ruvuma na Songea,”amesema Kalemani

Aidha, mradi huo wa umeme unatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 32,000 katika vijiji 120 vya mikoa hiyo, ambapo unatarajiwa kuwawezesha wananchi kuingiza fedha nyingi kutokana na fursa zitakazojitokeza baada ya kukamilika.

Hata hivyo, Kalemani amewataka Wakandarasi kumaliza kwa wakati mradi huo kwani tayari wameshapewa fedha zao bila kucheleweshewa, huku mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2018.

 

 

NEC yatoa orodha ya watakaogombea ubunge
Aina tata tano za ndoa