Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameteua viongozi wa taasisi mbalimbali wakiwemo Makatibu Wakuu, viongozi katika majeshi na mahakama.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, leo Januari 31, 2020 Rais Magufuli amemteua Mary Makondo Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Bi. Makondo ambaye awali alikuwa Kamishna wa Ardhi amechukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.
Aidha, Balozi Kijazi ameeleza kuwa Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo, Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo. Amechukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye pia amestaafu.
Wizara ya Viwanda na Biashara nayo imepata Katibu Mkuu mpya ambaye ni Profesa Riziki Silas Shemdoe ambaye awali alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma; akichukua nafasi ya Profesa Joseph Bucheshwaija ambaye amestaafu.
Wengini ni Bi. Zena Ahmed Said (Katibu Mkuu Wizara ya Nishati), Christopher Kadio (Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), Bw. Leonard R. Masanja (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati).
Wengine walioteliwa ni kama inavyoonesha sehemu ya Barua ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu: