Rais Dk. John Mgufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530, ambapo wafungwa 722 kati yao wameachiwa huru jana na 2,808 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki.

Rais ametoa msamaha huo katika kuadhimisha miaka 55 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika tarehe 26, April 1964.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani, Meja Jenerali Jacob kingu, imeeleza kuwa wafungwa wote watapunguziwa robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu cha 49 (1) cha sheria ya magareza.

Amesema msamaha huo, utawahusu wafungwa walio wagonjwa wa UKIMWI, Kifua kikuu na saratani, ambao wapo katia hali mbaya zaidi na watathibitishwa na jopo la madaktari chini ya mganga mkuu wa mkoa au wilaya husika.

Aidha msamaha huo pia utawahusu wafungwa wazee wenye umri wa mika 70 na kuendelea, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasio nyonyesha.

Wengine watakao nufaika na msamaha huo ni wale wenye ulemavu wa akili na mwili ambao wataangaliwa kwa umakini na madaktari.

Wafungwa ambao hawata nufaika na msamaha huo ni wale walio hukumiwa kunyongwa, au waliofanya makosa ya kujaribu kuua, kujiua au kuua watoto wachanga, waliohukumiwa kwa makosa ya kujihusisha na madawa ya kulevya, rushwa, unyang’anyi wa kutumia silaha, walawiti, wabakaji, waliofanya mashambulio ya aibu, kunajisi kulawiti, ukatili dhidi ya watoto, na waliowapa mimba wanafunzi.

Meja Jenerali Kingu, ameongeza kuwa wengine ambao hawatanufaika na msamaha ni wale wanaotumikia vifungo kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za serikali, kutoroka chini ya ulinzi, na wale wenye makosa ya kinidhanmu gerezani.

Watawa wawili kunyongwa kwa kumuua Askofu
LIVE: Ziara ya Rais Magufuli wilaya ya Chunya mkoani Mbeya