Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa wakifoji nyaraka za serikali.

Ameyasema hayo mapema hii leo mkoani Dodoma alipokuwa katika ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambapo amesema kuwa ni vyema vyombo vya usalama vikachukua hatua kali dhidi ya watu hao.

“Ni vyema watu wanaopotosha takwimu za taifa wakachukuliwa hatua kali zaidi, maana mtu akitoa habari ya kupotosha itakuwa ni gharama kubwa kuirudisa imani kwa wananchi,”amesema Dkt. Magufuli

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni bora watu hao wanaopotosha wakachukuliwa hatua kali ambazo zitawafanya wajifunze kutokana na makosa wanayoyafanya na kuwa mfano kwa wewngine.

 

Panga la moto kuwashukia wahubiri kwenye mabasi
Odinga amtunishia misuli Githu kuhusu kuapishwa