Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha mke wake Linah George Mwakyembe.
Katika salamu hizo, Rais Dkt. Magufuli amesema ameshtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, hivyo anaungana na familia ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Nakupa pole sana Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Linah, najua hisia za maumivu ulizonazo wwe na familia nzima, nyote nawaombea mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
Wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli amesali katika Ibaada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.
-
Maaskofu wamkingia kifua JPM, wanena mazito kuhusu mimba mashuleni
-
LIVE: Rais Dkt. Magufuli akipokea nyumba 50 kutoka taasisi ya Mkapa
-
JPM amteua Prof.Luoga kuwa mwenyekiti TRA
Hata hivyo, katika harambee hiyo amefanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 13 huku shilingi laki 920,000 zikiwa ni ahadi kutoka kwa watu mbalimbali walioshiriki katika ibaada.