Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, leo Novemba 10, 2018, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba.
Taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa nafasi ya Dkt. Charles Tizeba imeshikwa na Japhet Hasunga, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Aidha katika nafasi ya Waziri wa viwanda na biashara iliyokuwa chini ya Charles Mwijage, imechukuliwa na Joseph Kakunda, ambaye naye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa TAMISEMI.
Pia Rais Magufuli amemteua Constantine John Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, pamoja na kumteua Profesa Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora.
-
NEC yatoboa siri ya wabunge waliohama Chadema kupita bila kupingwa
-
Iwe kwa kutumwa au makusudi Ushoga ni mwiko Tanzania- Kangi Lugola
-
Nikisema Sukuma ndani sitanii, sasa naanza nawewe- RC Tabora
Rais Magufuli, amemteua, Innocent Lugha kuwa naibu Waziri wa Kilimo, pia amemteua Mwita Waitara kuwa naibu waziri wa TAMISEMI, na uteuzi wa viongozi unaanza Novemba 10, na wataapishwa Jumatatu Ikulu Jijini Dar es salaam.