Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewabadilikia baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano na kuwataka kutenda kazi kama atakavyo yeye kwani wasipofanya hivyo maana yake nafasi hizo haziwafai tena.
Ameyasema hayo wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko Ikulu jijini Dar es Salaam na kudai kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki pamoja na Naibu wake Stanslaus Nyongo na kuwataka kubadilika mara moja.
Bado Wizara ya Madini haifanya kazi vizuri sana najua nikizungumza kwa kupamba nitakuwa mnafiki Mhe. Spika utatambua mwezi wa 7 Bunge lilipitisha sheria ya madini kubadilisha ile sheria iliyokuwepo mkapitisha sheria namba 7 ya mwaka 2017 ambayo Bunge na Watanzania wengi tuliamini kwamba kupitia sheria hii mambo mengi ya nchi yangenyooka ikiwa pamoja na kupata mlahaba na kupata faida na madini yetu. Ile sheria ilipofika nilisaini na kuwapa maelekezo watendaji wangu kuandaa ‘regulations’ lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita regulations hazijasainiwa,”amesema JPM
Hata hivyo, Rais Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kutokana na vitendo hivyo vya wateule wake ni wazi kuwa kuna matatizo makubwa ndani ya Serikali.