Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Erasto Mfugale na Mwenzake wa Bukoba vijijini, Mwantumu Dau ambao watapangiwa kazi nyingine.
Viongozi hao walishindwa kutaja kiasi cha fedha za mfuko wa barabara zilizopokewa kwenye halmashauri zao walipoulizwa swali hilo katika uzinduzi wa uwanja wa ndege katika halmashauri hiyo.
Aidha, Wakurugenzi hao walipotakiwa kutaja kiasi cha fedha hizo zilizopokewa kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara walijibu kuwa wana idara nyingi wanazozisimamia hivyo si rahisi kukumbuka.
Akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua uwanja huo, Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali imetenga shilingi 159 bilioni ambazo zitatumika kulipa malimbikizo ya stahiki ya mishahara ya watumishi wa umma.
-
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii watakiwa kuongeza bidii
-
JPM kufanya ziara nchini Uganda
-
LIVE: Rais Magufuli katika akizinduzi uwanja wa ndege Kagera
Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli ameagizwa kuchunguzwa kwa watumishi 110 waliowasilisha madai hewa wachunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaobainika kufanya hivyo kwa makusudi.