Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewatakia watanzania wote heri ya mwaka mpya 2018, huku akiwataka kuendelea kuchapa kazi.

Ametoa ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa twitter ambapo ameweka picha yenye ujumbe huo wa mwaka mpya, na kuwaomba Watanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano, sambamba na kufanya kzi kwa bidii ili kujenga nchi.

“Ndugu zangu Watanzania, nawatakia heri ya mwaka mpya 2018, naungana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake, nawaomba tuendelee kudumisha amani, upendo, mshikamano wetu na tuchape kazi kwa juhudi na maarifa, kwa maendeleo ya Taifa letu ili tujenge Tanzania mpya, umeandika ujumbe huo Rais Dkt. Magufuli

 

Maalim Seif: JPM ameirejesha nidhamu ya nchi
Zitto: Tukio la Lissu lilinigharimu