Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Mabalozi wote nchini kuondoka kuelekea katika vituo vyao vya kazi pindi wanapoapishwa.

Ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam  wakati wa hafla ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola, ambapo ameonesha kuchukizwa na suala la baadhi ya mabalozi kuchelewa katika vituo vyao vya kazi baada ya kula kiapo Ikulu.

“Kuna Balozi wa Zambia nimemteua, kila siku namuona anazunguka kwenye ofisi anaaga, mara kwa Waziri Mkuu, mara kwa Makamu wa Rais, mara Zanzibar, mwache aendelee kuaga, aende na kwa wakuu wa mikoa, akimaliza kuaga, Ubalozi atakuwa umeishia hapo”, amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Balozi Hassan Simba Yahya aliapishwa na Rais Magufuli Machi 4, 2019 Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo baada ya kula kiapo hicho, Machi 18 Balozi alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kuaga tayari kwenda kuanza kazi kwenye kituo chake kipya.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Machi 29, 2019
Masharti ya Ariana Grande yawachefua waandishi, watishia kumsusia