Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa Tanzania inahitaji sana wawekezaji kuja kuwekeza nchini lakini wawekezaji ambao wanajifanya kuja kuwekeza kwa kigezo cha kuiba mali za nchi hawatakiwi na bora wasije kabisa nchini.

Amesema hayo akiwa ziarani Mkoani Manyara wilaya ya Simanjiro wakati akizindua barabara na kusema wawekezaji ambao wanataka kuja kuwekeza ili kuiba rasilimali za nchi ni bora wasije kwani hawatafanikiwa chini ya utawala wake wa awamu ya tano.

“Tanzania tunahitaji wawekezaji lakini si wawekezaji wanaotaka kutuibia, kama unataka kuja kuwekeza Tanzania kwa kisingizio cha kuja kutuibia ni bora usije, kwani utakuwa umeula wa chuya kwa sababu wakati huu hautaiba, nasema huyo mwekezaji atalia na hili nalisema kwa uwazi kwa sababu tumeamua kupambana kwa ajili ya vita ya uchumi kwa ajili ya taifa letu,”amesema Rais Dkt. Magufuli 

Hata hivyo, amesema kuwa kuwa mataifa makubwa na wawekezaji kutoka nje wamewajengea mawazo kuwa wao ndiyo wenye mali na uwezo kumbe wao hawana hizo mali na uwezo bali Watanzania ndiyo wenye mali na uwezo huo kuliko wao ambao wanategemea maliasili za Watanzania.

 

NEMC yaipiga faini garage bubu jijini Dar
Zitto Kabwe akamatwa na Jeshi la Polisi Dar