Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepinga baadhi ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji wa kongamano la mwenendo wa uchumi na siasa ndani ya miaka mitatu ya awamu ya tano, ikiwemo hoja iliyosema kwamba asilimia kubwa ya wateule wa Rais wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka yao.

Makonda amesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaolalamika matumizi mabaya ya wateule hao wa Rais walikuwa wanufaika wa mfumo mbovu.

“Rais hajamtuma RC na DC kutumia mamlaka vibaya, kupima utendaji wa Rais Magufuli ni kama kutoa treni barabarani kuirudisha kwenye reli, kwa hiyo lazima kuna vyuma lazima vitalalamika, niwaombe tusichukulie matukio machache yanatokea kuwa ni maagizo ya Rais,” amesema Makonda.

Aidha, awali mbunge mteule wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam, Mwita Waitara amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuangalia upya namna ya kuzalisha ajira kwa vijana ili kupunguza vilio vya ajira.

Akichangia kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka 3 cha serikali ya awamu tano, Waitara amesema kuwa suala la ajira kwa wananchi wa Tanzania lipewe kipaumbele.

Video: Magufuli aanika utajiri Tanzania, Mbowe azidiwa...
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 2, 2018