Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri wa Muungano Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa upinzani utavurugika baada ya wanachama, wabunge na madiwani kuanza kuhamia chama tawala.

Ameyasema hayo hii leo kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao unaofanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwepo marais wastaafu.

“Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli kweli,”amesema JPM

Aidha amewataka viongozi wapya wa Chama hicho kuhakikisha wanafanya kazi ya kuongeza wanachama wapya katika chama hicho ili kiweze kuwa imara zaidi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wataendelea kupokea na kuwatangaza watu ambao wanahamia kwenye chama hicho, na kusema kuwa lazima kwanza wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana mpango mzuri kwa CCM

 

Salim Mbonde kurejea dimbani, asisitiza ligi ngumu
Heche: Serikali haijawahi kupambana na rushwa