Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa ana wajibu mkubwa wa kuzisimamia jumuiya zilizopo ndani ya CCM.

Ameyasema hayo mapema hii leo mjini Dodoma alipokuwa akihutubia katika mkutano wa 9 wa Jumuiya ya wazazi Tanzania, huku akiwatakia mkutano mwema.

“Tembeeni vifua mbele kwani jumuiya hizi siwezi kuzitupa, na ninawajibu mkubwa sana wa kuzisimamia na kuzihudumia,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amewatakia uchaguzi mwema na kutahadharisha wagombea kutojishughulisha na vitendo vya rushwa.

Magufuli awatahadharisha mabinti watembea utupu
Mwambusi ailaumu TFF kushindwa kwa Timu ya Taifa