Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, amesema kuwa anakumbuka jinsi aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga alivyomsumbua kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Usagara, ambayo hapo mwanzo haikuwepo.

Dkt. Magufuli amesema hayo leo Septemba 8, 2020, akizungumza na wakazi wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, wakati akimnadi mgombea wa sasa wa jimbo hilo, Alexander Mnyeti katika eneo la Usagara.

Mimi nataka tu nieleze ukweli,  nilikuwa na Mbunge hapa Kitwanga, alikuwa ananisumbua sana, baadhi ya miradi nataka kuwaeleza mipango iliyofanyika hapa ni mingi hata hii Barabara haikuwepo katika kipindi cha miaka mitano tuliifanya na aliyenisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni alinisumbua sana ujenzi wa barabara hiyo“, amesema Dkt. Magufuli.

Zlatko: Wazawa Young Africans kikwazo
Sven: Kilichotukuta kwa Ihefu FC nilikitarajia