Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru  Ally ameeleza ratiba ya awamu ya sita ya mgombea urais wa chama hicho , Dkt John Magufuli ,na kueleza sababu za kwa nini hatakwenda baadhi ya mikoa kuomba kura .

Akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi ndogo za makao makuu ya CCM jijini Dar es Salaam kuwa Magufuli hatakwenda katika mikoa mingine kutokana na ufinyu wa muda na hasa baada mgombea mwenza ,Samia Hassan na mjumbe wa kamati kuu Kassim Majaliwa, kufika katika maeneo ambayo mgombea urais hakufika.

“Mgombea urais asingeweza kufika maeneo yote nchini, lakini ukiunganisha ratiba ya Rais Magufuli na mgombea wa Zanzibar, Mjumbe wa kamati kuu Majaliwa ,mgombea mwenza Mama Samia ,utaona kote tumeenda.

Hivyo mgombea urais akitoka Dar es Salaam anaenda Pwani, Tanga kisha atakwenda Kilimanjaro ,ataingia Arusha,Manyara na kisha ataingia Dodoma,” amesema Bashiru.

Bashiru amesema baadhi ya mikoa ukiwemo Katavi na Rukwa amemtuma makamu wa rais kwa mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na pemba atamtuma Waziri mkuu Majaliwa  na Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Jakaya Kikwete .

Watoto wa miaka 14 wadaiwa kubaka
Maalim Seif afungiwa kufanya kampeni