Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajia kupokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almas uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema kuwa, ripoti hiyo itakabidhiwa kwa Rais Dkt. Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya hii leo kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Spika wa Bunge.

Hata hivyo, Hafla hiyo ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo inatarajiwa kurushwa hewani na vyombo mbalimbali vya habari ili kuweza kuwafikia wananchi wote.

t

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 7, 2017
Viingilio mchezo wa Azam FC v Simba SC