Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Januari 27, 2021 anatarajiwa kuzindua shamba la miti wilayani Chato mkoani Geita lenye ukubwa wa hekta elfu 69.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa  tukio hilo litafanyika katika eneo la Butengo wilayani Chato mkoani Geita.

Amesema kuwa uanzishwaji na uendelezwaji wa shamba hilo unaenda sambamba na malengo ya Serikali ya kuhifadhi mazingira na kuinua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali za misitu.

Gabriel amesema mradi huo wa upandaji miti ambao serikali imewekeza unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi mazingira na kuchangia uhifadhi wa misitu katika Kanda ya ziwa na nchi kwa ujumla.

Shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 69,000 ni la Pili kwa ukubwa baada ya shamba la miti Saohill lenye ukubwa wa hekta 135,900 ni miongoni mwa mashamba 23 ya Serikali yanayosimamiwa na kuendelezwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS).

Rais Karia awashukia mashabiki
Waziri awaonya wanaotoa taarifa za wateja makampuni ya simu